Demi Moore
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Demi Gene Guynes (amezaliwa tar. 11 Novemba 1962) anafahamika kwa jina la kikazi kama Demi Moore, ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani.
Baada ya nyusika ndogondogo katika filamu na maigizo ya vipindi vya televisheni General Hospital, Moore amekuza kazi yake katika filamu kama vile St. Elmo's Fire (1985) na Ghost (1990) na mwanzoni mwa miaka ya 1990 amekuwa miongoni mwa waigizaji wa kike wenye kulipwa mapesa mengi sana katika Hollywood kwa kufuatia mafanikio yake katika filamu kama vile A Few Good Men (1992), Indecent Proposal (1993) Disclosure (1994). The Hunchback of Notre Dame (1996) na G.I. Jane (1997). Mwishoni mwa miaka ya 1990 filamu zake zilikuwa na mafanikio machache, lakini amerudi tena katika umaarufu na uhusika wake katika Charlie's Angels: Full Throttle (2003).
Moore amechukua jina lake la kikazi kutoka kwa mume wake wa kwanza Freddy Moore na ni mama wa watoto watatu kutoka katika ndoa yake na Bruce Willis. Baada ya kuolewa na mwigizaji Ashton Kutcher mwaka 2005 alibadili jina lake la mwisho kuwa Kutcher mnamo 2009.
Remove ads
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads