Dibaji

From Wikipedia, the free encyclopedia

Dibaji
Remove ads
Remove ads

Dibaji (kutoka neno la Kiarabu; pia "kilemba") ni kipande cha maandishi (kwa kawaida huwa kifupi) ambacho huwekwa mwanzoni mwa kitabu au kazi nyingine za fasihi.

Thumb
Dibaji ya kitabu cha "Men I Have Painted" cha John McLure Hamilton; 1921.
Thumb
Dibaji ya kitabu cha mwaka 1900 katika lugha ya Kijerumani.

Hasa huandikwa na mtu mwingine, mbali na mwandishi halisi wa kitabu. Huelezea mahusiano na mwingiliano wa kazi zao na mwandishi mkuu au huelezea lilelile linalohusiana na kitabu, kama vile nia na manufaa yake.

Kwa utaratibu huu, wakati mwingine, si lazima sana katika matoleo ya baadaye kukatokea dibaji nyingine mbali na ile ya awali (hutokea kabla ya nyingine kama mwanzo ilikuwepo), hili huweza kuelezea kwa nini matoleo hayo mawili hutofautiana.

Dibaji ikiandikwa na mwandishi mwenyewe, basi huelezea namna kitabu kilivyotengenezwa, na wazo limetokea wapi, na huenda ikajumuisha na shukrani kwa watu waliosaidia uundwaji wa kitabu.[1] Tofauti na tabaruku, dibaji kwa kawaida lazima iwe imesainiwa.

Maelezo ya msingi yanayohusu matini makuu ya kitabu kwa kawaida hujipambua vilivyo, au hasa utangulizi, tofauti na dibaji au tabaruku.

Remove ads

Tazama pia

Marejeo

Loading content...

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads