Dini za Abrahamu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Dini za Abrahamu, ni dini zenye asili katika Mashariki ya Kati ambazo zinashika imani katika Mungu mmoja tu.[1]


Asili
Dini hizo zinamchukua Abrahamu kama kielelezo cha mwamini na rafiki wa Mwenyezi Mungu.[2][3] Dini kuu za jamii hiyo (kadiri ya tarehe ya kutokea) ni: Uyahudi (KK), Ukristo (karne ya 1 BK) na Uislamu (karne ya 7),[4][5][6][7] mbali na nyingine ndogo zaidi zilizotokana nazo, kama Baha'i (karne ya 19).
Uenezi
Inakadiriwa kwamba 54% za watu wote duniani wanafuata mojawapo kati ya dini hizo, zikiwemo: Ukristo (33%), Uislamu (21%) na Uyahudi (0.2%).[8][9]
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads