Do You

From Wikipedia, the free encyclopedia

Do You
Remove ads

"Do You" ni wimbo wa 2007 ulioimbwa na mwimbaji-mtunzi wa R&B Ne-Yo. Wimbo unamzungumzia Ne-Yo akiwa anajaribu kumwuliza mwanamke wake wa zamani kuwa keshawahi kumfikiria kabisa. Ni wimbo wa pili kutoka katika albamu yake ya pili ya Because of You.

Ukweli wa haraka Imetolewa, Muundo ...

Wimbo ulitolewa rasmi katika maredio kunako tarehe 12 Juni 2007. Katika mahojiano yake na BET, Ne-Yo amesema kwamba wimbo wa "Do You" ni sehemu ya pili ya wimbo wake wa awali wa "So Sick" ambao unatoka katika albamu yake ya kwanza ya In My Own Words.[1]

Remix ya wimbo huu amemshirikisha mwanamama Mary J. Blige. Na remix yake nyingine amepata kumshirikisha mwanadada mwingine aitwaye Hikaru Utada, ambao ulitolewa nchini Japan kunako 21 Novemba 2007 ikiwa kama mmoja kati ya wimbo wa 7 kwa tungo zake za Kiingereza kutoka kwa mwanadada huyo.

Remove ads

Video yake

Mwanzoni kabisa Ne-Yo anaonekana akipigana na mpenzi wake wa zamani katika gari, ambaye baadaye aliondoka zake. Ne-Yo akawa anajaribu kuandika barua kwa mpenzi wake huyo huku akiwa anajaribu kumwuliza kama ana mkumbuka.

Inaonekana kuwa ni vigumu kwa yeye kumkumbuka, na baadaye akapata kusoma barua aliyotumiwa na Ne-Yo na akaamua kuikunja-kunja na kuitupilia mbali. Mpenzi huyo baada ya muda anaonekana kumpiga busu mpenzi wake mpya wakiwa katika kochi, na akiwa amemlalia mapajani, wakati huohuo akiwa amemkalia mbali kidogo.

Ne-Yo kisha akakumbuka sehemu ambayo alikuwa ana kawaida ya kumpiga busu mpenzi wake huyo katika kochi hilohilo alilokaa na huyo bwana mpya. Ne-Yo akaonekana akiendesha gari kwa kasi kisha akalisimamisha katika eneo lenye kibanda cha kupigia simu za kulipia, na kuanza kumpigia simu mpenzi wake wa zamani aje katika eno lile la kibanda cha simu za kulipia. Lakini kwa kwa bahati mbaya ule muda ambao dada yeye kafika, Ne-Yo yeye akawa tayari kesha ondoka zake.

Remove ads

Chati

Maelezo zaidi Chati (2007), Nafasik Iliyoshika ...

Remix aliyoimba na Hikaru Utada

Mauzo ya Digital na Chati za Ujapani

Maelezo zaidi Chati, Nafasi iliyoshika ...
Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads