In My Own Words
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
In My Own Words ni albamu ya kwanza ya mwimbaji-mtunzi wa R&B Ne-Yo. Albamu ilitoka mnamo tar. 28 Februari 2006. Nyimbo nne zilipata kutolewa katika albamu hii, "Stay", "So Sick", "When You're Mad", na "Sexy Love".
Wimbo wa kwanza kutolewa ulikuwa, "Stay", lakini hakumpa mafanikio makubwa na kuufanya kuwa wimbo pekee wa Ne-Yo, ambao haukupata kufikia chati za Billboard Hot 100 bora. Albamu ilipata kushika nafasi ya kwanza katika Billboard 200 kwa kuuza nakala zipatazo 301,000 katika wiki ya kwanza.
Badala ya hapo, kunako mwezi Agosti 2006, Ne-Yo akaanza kufanya matamasha na kuzunguka katika miji ya mbalimbali huku akiwa na baadhi ya wasanii wenzake kama vile Chris Brown na Dem Franchize Boyz. Baadaye albamu ikafikia kiwango cha platinam 1 kwa kuuza nakala mil. 1.6 kwa Marekani, na kopi milioni 2 kwa mauzo ya dunia nzima.
Remove ads
Maelezo
Ne-Yo ndiyo alioandika nyimbo za albamu nzima. Watayarishaji wa Kinorwei (Stargate) wametayarisha wimbo wa, "So Sick", na pia wamechangia mawili-matatu katika wimbo wa "Sexy Love", "Let Go", na "Time" kwa ajili ya LP ya kwanza.
Watayarishaji wengine katika albamu hii ni kama vile Ron "Neff-U" Feemstar, Brain "B-Nasty" Reed, na Jai "King" Titus of Drama Family Entertainment, ambaye ametayarisha wimbo wa kwanza, "Stay", na "Sign Me Up". "Let Me Get This Right" ni kazi nyingine ya wana Drama Family Entertainment.
Remove ads
Orodha ya nyimbo zilizopo
Remove ads
Chati
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads