Elibariki Emmanuel Kingu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Elibariki Emmanuel Kingu ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha Chama Cha Mapinduzi (CCM). Amechaguliwa kuwa mbunge wa Singida Magharibi kwa miaka 20152020. Alimuomba Makamu wa Rais Samia Suluhu kuwa amsaidie apitishwe na CCM kugombea 2020 bila kupingwa ndani ya chama chake. Anapingana kwa wazi na wanasiasa wa CHADEMA na ACT Wazalendo[1].

Pia amewahi kupita nafasi ya Mkuu wa Wilaya Kisarawe na Mkuu wa Wilaya Igunga kabla ya kuingia bungeni kuwakilisha Singida Magharibi kwa vipindi viwili yaani mwaka 2015-2020 na 2020-2025.

Elibariki Kingu amejitanabaisha kuwa ni mwanasiasa wa kimkakati kwani ni Mjumbe wa Bunge la Kimataifa (IPU) aliyeshiriki kikamilifu kwenye kampeni za kumchagua Rais wa mabunge duniani Bi Tulia Ackson na kushinda mnamo mwaka 2024. Pia kwa nafasi yake ya ujumbe wa IPU alishiriki kikamilifu kwenye kampeni za kuchaguliwa Marehemu Dkt Faustine Ndungulile kwenye nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa WHO kanda ya Africa na kuweka historia ya kipekee kuwa mtanzania wa kwanza kwenye nafasi hiyo.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads