Msokotaji-hariri

From Wikipedia, the free encyclopedia

Msokotaji-hariri
Remove ads

Wasokotaji-hariri ni wadudu wadogo wa oda Embioptera (embios = -epesi, ptera = mabawa) ambao wana tezi kwenye miguu ya mbele zinazotumika kwa kusokota hariri. Hutumia hariri hii ili kuumba njia na vyumba juu ya miamba, juu ya gome la miti au ndani ya takataka za majani. Mwili wa wadudu hawa ni kinamo na una umbo wa mcheduara. Hii inarahisisha maisha yao ndani za njia za hariri. Madume ya spishi nyingi wana mabawa lakini madume ya spishi nyingine na majike wote hawanayo.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Wasokotaji-hariri huishi ndani ya njia za hariri takriban saa zote. Madume wanatoka njia hizi ili kutafuta majike, na majike wanatoka ili kutafuta chakula. Wakipata chakula majike wanaumba njia mpya za hariri juu ya chakula hiki. Hula takataka za majani, vigoga, gome na kuvumwani. Madume hawakuli.

Remove ads

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki

  • Chirembia baringoa
  • Chirembia leechi
  • Chirembia micropallida
  • Dihybocercus confusus

Picha

Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Msokotaji-hariri kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hiyo kuhusu "Msokotaji-hariri" inatumia jina ambalo halijakuwepo kwa lugha ya Kiswahili. Jina hili linapendekezwa kwa jina la mnyama huyu au wanyama hawa amba(ye)(o) ha(wa)na jina kwa sasa.

Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.

Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads