Epikur

From Wikipedia, the free encyclopedia

Epikur
Remove ads

Epikur (kwa Kilatini na lugha mbalimbali Epicurus, kutoka Kigiriki Ἐπίκουρος, Epíkouros, yaani "Mwenzi"; 341270 KK) alikuwa mwanafalsafa wa Ugiriki wa Kale, maarufu kama mwanzilishi wa shule ya falsafa yenye jina lake (kwa Kiingereza: Epicureanism).

Thumb
Sanamu ya Kirumi ya Epicurus.

Maandishi

Kati ya maandishi yake 300 hivi, zimebaki tu sehemu na barua chache; zaidi tunajua kutoka kwa wafuasi wake na wengineo waliofafanua mafundisho yake.

Mafundisho

Kwake, lengo la falsafa ni kufikia maisha yenye heri, utulivu, amani, kutoogopa, kutoteseka, kujitegemea na kuzungukwa na marafiki. Kwake raha na maumivu ndio vigezo vya uadilifu au uovu wa mambo yoyote. Pia kifo ni mwisho wa mwili na roho, hivyo hakitakiwi kuogopwa. Tena hakuna miungu ambao waadhibu wala kutuza binadamu. Ulimwengu hauna mipaka na ni wa milele.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads