Ermengol wa Urgell
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ermengol wa Urgell (pia: Armengol au Armengod au Hermengaudius; alifariki El Pont de Bar, 1035) alikuwa askofu wa Urgell kuanzia mwaka 1010.


Mtoto wa ukoo tawala[1][2], alianza uaskofu wake kwa kurekebisha maisha ya mapadri wa kanisa kuu kufuatana na mafundisho ya Agostino wa Hippo
Anatajwa kama mhusika wa kuteka mji wa Guissona mwaka 1024 na kuurudisha kwenye Ukristo.
Alishindana mara nyingi na masharifu wa Urgell na kuwajibika katika ujenzi wa miundombinu, likiwemo kanisa kuu la Urgell. Akiwa anafanya kazi kwa mikono yake kujenga daraja, alianguka chini akavunjika kichwa kwenye mawe [3].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads