Eustasi White

From Wikipedia, the free encyclopedia

Eustasi White
Remove ads

Eustasi White (Louth, Uingereza, 1559 London, 10 Desemba 1591) alikuwa Mkristo wa Kanisa la Anglikana kabla hajajiunga na Kanisa Katoliki.

Thumb
Mt. Eustasi (wa pili kutoka kulia) na wenzake.

Baada ya kuhamia Ulaya bara, aliingia seminari kwa lengo la kurudi kwao kufanya uchungaji usioruhusiwa na serikali, akapewa daraja ya upadri (1588).

Hapo alirudi Uingereza lakini baada ya muda mfupi aliuawa kwa kunyongwa na kukatwa vipandevipande chini ya sheria[1].

Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39.

Sikukuu yake ni tarehe ya kifodini chake[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads