Ewostatewos
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ewostatewos (kwa Kigeez: ኤዎስጣቴዎስ, ʾĒwōsṭātēwōs, au ዮስጣቴዎስ, Yōsṭātēwōs, kutoka Kigiriki Εὐστάθιος, Eustathios; 15 Julai 1273 – 15 Septemba 1352 kadiri ya Kalenda ya Juliasi) alikuwa mmonaki, mwalimu wa Absadi.
Alidai utekelezaji wa Sabato pamoja na Dominika katika Ukristo wa Ethiopia. Hatimaye wafuasi wake walifaulu kufanya msimamo huo ukubaliwe mwaka 1450 kwenye Mtaguso wa Debre Mitmaq huko Tegulet.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia na Kanisa la Kiorthodoksi la Eritrea kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Chanzo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads