Flavour
Mwanamuziki wa Nigeria From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Chinedu Okoli (anajulikana zaidi kwa jina la kisanii Flavour N'abania au kwa kifupi Flavour; alizaliwa Jimbo la Enugu, 23 Novemba 1983) ni mwimbaji wa Nigeria.
Maisha ya awali
Flavour, anayejulikana kwa uwezo wake wa kuimba kwa ufasaha katika Lugha ya Kiigbo,[1] alizaliwa katika eneo la kusini mashariki mwa Nigeria. Asili ya familia yake ni kutoka Umunze katika Halmashauri ya Serikali za Mitaa ya Orumba South, Jimbo la Anambra, kusini mashariki mwa Nigeria.[2] Flavour alianza taaluma yake ya muziki akiwa na umri wa miaka 13, alipokuwa akiimba nyimbo za kwaya katika kanisa allokua akisalia mjini Enugu, Jimbo la Enugu. Mchungaji wa kanisa lake alimjulisha kwa rafiki yake, Chris I. Ordor, Mkurugenzi Mtendaji wa SoundCity Communications. Mwaka wa 1996, Flavour alialikwa kujiunga na kampuni hiyo kupitia ufadhili wa masomo ili kusomea muziki.
Baada ya miaka mitatu ya kupiga ngoma, Flavour alianza kupiga ngoma kitaalamu. Mnamo 1999, aliacha kupiga ngoma na kuanza kupiga kinanda.[3] Pia aliwahi kutoa sauti za nyuma kwa wasanii wengine katika SoundCity.[4]
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads