Forest (Mbeya mjini)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Forest ni kata ya Mbeya Mjini katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania yenye Postikodi namba 53103.
Forest iko ng'ambo ya barabara kuu ya TANZAM kati ya Mwanjelva na Mabatini. Imeanzishwa tangu miaka ya 1980 katika eneo lenye msitu wa milingoti ulioanza kando ya barabara kuu ukitazama Mabatini. Shabaha ya kuanzisha eneo hili ni kuwa na kitovu kipya cha manispaa ya Mbeya kwa sababu mji wa kale hauna nafasi tena kwa upanuzi wa huduma za serikali na biashara.
Kati ya majengo ya kwanza ya Foresti, mojawapo lilikuwa hospitali ya mkoa.
Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 9,774 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,649 [2] walioishi humo.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads