Forodha
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Forodha (ing. customs) ni jina la mamlaka ya nchi inayosimamia kuingia na kutoka kwa bidhaa zikivuka mipaka. Tangu kale kazi yake ni hasa kukagua thamani ya bidhaa na kudai malipo ya ushuru[1] ambayo ni pesa inayokadiriwa kama sehemu ya thamani ya bidhaa kwa kibali cha kuzileta au kuzitoa nchini.[2]


Kwa hiyo vituo vya forodha hupatikana kwenye mpaka wa nchi, pamoja na bandarini, uwanja wa ndege na ofisi za posta kwa vifurushi kutoka nje.
Kazi muhimu ya forodha ni pia kudhibiti bidhaa haramu kama madawa ya kulevya au bidhaa hatari ambako ni lazima kuhakikisha zinasafirishwa kwa njia salama, pamoja na hati zinazoonyesha maudhui yake kikamilifu.
Nchini Tanzania forodha ni sehemu ya Mamlaka ya Mapato ya Tanzania chini ya kamishna wa ushuru wa forodha na bidhaa.
Remove ads
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads