Yohane wa Fiesole

From Wikipedia, the free encyclopedia

Yohane wa Fiesole
Remove ads

Yohane wa Fiesole, O.P. au Beato Angelico (yaani, kwa Kiitalia: "Mwenye heri wa Kimalaika"[2]; jina la awali: Guido di Pietro; Vicchio, Firenze, 1395 hivi[3]Roma, 18 Februari 1455) alikuwa mtawa padri maarufu kama mmojawapo wa wachoraji wa kwanza wa Renaissance nchini Italia. Mtaalamu Giorgio Vasari katika kitabu chake Maisha ya Wasanii aliandika kwamba alikuwa na "kipaji adimu na kamili".[4]

Thumb
Sura yake katika mchoro Matendo ya Mpingakristo, kazi ya Luca Signorelli (1501 hivi), kanisa kuu la Orvieto, Italia[1].
Thumb
Mchoro wake: Bikira akipashwa habari.
Thumb
Mchoro wake: Kristo msulubiwa.
Thumb
Hukumu ya mwisho, mchoro wake juu ya altare ya kanisa la San Marco, Florence.
Thumb
Kugeuka sura, mchoro wake katika chumba cha mtawa.
Thumb
Mkombozi akibariki, mchoro wa mwaka 1423.
Thumb
Bikira na Mtoto pamoja na Watakatifu, sehemu ya mchoro, Fiesole (14281430)

Tarehe 3 Oktoba 1982 Papa Yohane Paulo II alimtangaza rasmi kuwa mwenye heri,[5] kutokana na utakatifu wa maisha yake, si tu kwa kipaji chake cha kutoka mbinguni.[6]. Vasari huyohuyo aliandika kwamba "haiwezekani kumsifu mno baba huyo mtakatifu, aliyekuwa mnyenyekevu na mtaratibu hivi katika yale yote aliyoyafanya na aliyoyasema, na ambaye picha zake zilichorwa kwa unyofu na ibada kubwa hivi."[4]

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads