Fuwawe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Fuwawe (pia: fuwe; ing. pumice) ni aina ya mwamba mwepesi inayoundwa na povu ya zaha.


Maana yake zaha, ambayo ni mwamba joto sana katika hali ya kiowevu, inarushwa kutoka volkeno kwa shinikizo kubwa na inakuwa kama povu kwa sababu shinikizo linapungua haraka sana. Ikipoa haraka umbo hilo linaganda kuwa thabiti na kubaki vile.
Kwa hiyo asili ya fuwawe ni daima mlipuko wa volkeno.
Fuwawe inatokea kama mkusanyiko wa vipande-vipande au pia kama maganda manene.
Mara nyingi ni nyepesi kiasi kwamba inaelea juu ya maji, angalau kwa muda hadi maji yanapoingia na kujaza polepole nafasi ndani yake.
Kitamaduni inatumiwa kwa kusugua na kusafisha ngozi. Fuwawe iliyosagwa inatumiwa pia kwa kusafisha meno kwa msaada wa mswaki.
Kuna pia matumizi ya fuwawe kwa ujenzi maana ni kifaa chepesi chenye tabia nzuri za kuhami dhidi ya baridi na joto. Kwa kawaida inapondwa na kuchanganywa na kiasi kidogo cha saruji[1] lakini kuna pia majaribio ya kuitumia vile.[2]
Remove ads
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads