Mswaki
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Jina hilo ina linaweza kutumiwa tofauti angalia Miswaki (kata ya Uyui)



Mswaki (kutoka Kiarabu سواك, miswaq) ni kifaa cha kusafishia meno, ulimi na ngozi ndani ya mdomo.
Mswaki asilia
Kimapokeo mswaki ni kijiti kibichi ambacho kinatokana na mti au kichaka na kisha kutafunwa upande mmoja kinatumika kusafishia meno kutoka mabaki ya chakula yanayoweza kuharibu meno.
Hasa ukitokana na mti mswaki (Salvadora persica) (arak kwa Kiarabu) au miti mingine maalumu kadiri ya mazingira, kwa mfano msega au mkupa (Dobera glabra na D. loranthifolia), una sifa za muda mrefu zinazoufanya uendelee kuwa mbadala wa miswaki ya kisasa, ikiwepo ile inayotumia umeme.
Inasemekana mswaki unaimarisha ufizi (nyama inayoshikili meno), unazuia uozo wa meno, unaondoa maumivu ya meno na harufu mbaya kinywani.
Remove ads
Uenezi
Unatumika hasa Uarabuni, Afrika Kaskazini, kwenye Sahel na Pembe ya Afrika, India, Asia ya Kati, Asia ya Kusini Mashariki.
Sayansi inasemaje
World Health Organization (kifupi WHO, yaani Shirika la Afya Duniani chini ya Umoja wa Mataifa) ilihamasisha matumizi ya mswaki mwaka 1986.
Mwaka 2000 ripoti ya kimataifa kuhusu usafi wa kinywa ilionyesha makubaliano ya kwamba unahitajika utafiti zaidi kuthibitisha faida ya mswaki.[1]
Siku hizi watu wengi hutumia miswaki ya kisasa iliyotengenezwa kiwandani yenye shikamano, kichwa na nywele ngumu, kwa kawaida yote ya plastiki, pamoja na dawa ya meno. Utafiti wa mwaka 2003 ulionyesha kwamba matumizi sahihi ya mswaki asili yalikuwa na manufaa kuliko miswaki ya kisasa.[2] Hata hivyo, utafiti uliishia kupima watu 15 tu, idadi isiyotosha kabisa kama uthibitisho wa kisayansi.
Matumizi
Ingawa wengi wanapiga mswaki hasa asubuhi wanapooga au kunawa, halafu pengine huenda wakanywa chai ambayo inaacha sukari katika meno na hivyo kuandaa uozaji wake, utaratibu sahihi ni kupiga mswaki baada ya chakula, hasa cha jioni, kusudi meno yabaki safi muda wote wa usiku.
Kwa kulinda usafi, ncha ya mswaki inatakiwa kukatwa kila unapotumika.
Usitunzwe kamwe karibu na choo au sinki.
Mswaki ukikauka unatakiwa kulainishwa kwa maji ya waridi.
Remove ads
Katika Uislamu
Una nafasi muhimu vilevile katika sheria za Uislamu[3] kutokana na hadithi mbalimbali kusimulia kwamba Mtume Muhammad alikuwa anausifu:[4][5]
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads