Gamalieli

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Gamalieli alikuwa kiongozi wa kabila la Manase anayetajwa katika Biblia ya Kiebrania, ambayo ni sehemu ya Biblia ya Kikristo (Agano la Kale), katika kitabu cha Hesabu, sura ya 2, mstari wa 20.

Muhimu zaidi ni Gamalieli mwingine, Gamalieli I au Gamalieli mzee, kiongozi wa Mafarisayo katika karne ya 1 B.K. Anatajwa katika Agano Jipya, ambayo ni sehemu ya pili ya Biblia ya Kikristo, kama mwalimu wa mtume Paulo aliyewatetea mitume wa Yesu. Katika Mdo 5:34-39 anaonekana kama msemaji wa Mafarisayo na Mwalimu wa Torati anayepinga jitihada za Masadukayo kuua Petro na mitume wengine.

Kutokana na taarifa hiyo mapokeo ya Ukristo yanamheshimu kama mtakatifu. Katika Talmud ya Uyahudi anatajwa kwa heshima kama Rabban Gamliel.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads