George Miok

From Wikipedia, the free encyclopedia

George Miok
Remove ads

George "Gyuri" Miok (18 Mei 1981 - 30 Desemba 2009) alikuwa sajenti wa Kikosi cha Ulinzi cha Kanada. Aliuawa akiwa vitani huko nchini Afghanistan mnamo 2009. Alizawadiwa nishani kadhaa na Canadian Peacekeeping Service Medal, NATO Medal for Former Yugoslavia na South-West Asia Service Medal.

Thumb
Marehemu George Miok

Maisha ya awali

George (au György) alizaliwa katika familia ya Wakanada-Wahungaria mjini Edmonton, baba'ke alikuwa Illés Miok (kutoka Senta, Voivodina), mama'ke alikuwa Anna Miok (kutoka Jimbo la Veszprém), alikuwa na ndugu watatu, Michael, John na László.[1][2][3][4] Hakuoa wala kuwa na watoto.

Alikuwa mwalimu, alisoma katika Chuo Kikuu cha Alberta.[5] Mnamo mwaka wa 2008-2009 alifundisha masuala ya kidini, hesabu, mambo ya mazoezi kwenye jim kwa ajili ya wanafunzi wa daraja la 7 katika shule ya St. Cecilia's Junior High School mjini Edmonton.[6]

Alikuwa mwanachama wa jumuia ya Wahungaria wa Edmonton, pia alikuwa akiongea Kihungaria.

Remove ads

Kazi ya jeshi

Miok alijiunga na jeshi akiwa na umri wa miaka 17. Mnamo mwaka wa 2002 alienda zake nchini Bosnia kutumikia kwenye Kikosi cha Udhibiti.[7] Alikwenda nchini Afghanistan kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 2005. Alikuwa mwanachama wa 41 Combat Engineer Regiment na alikuwa akitumikia katika Kikosi cha Kujenga Upya cha Mkoa wa Kandahar.[8][9] Mnamo mwaka wa 2009, yeye na wanajeshi wengine watatu wa Kikanada walikufa, baada ya gari lao la silaha kupigwa na bomu la kubuni kilomita nne kutoka kusini mwa Jiji la Kandahar.[10][11][12] Alikuwa mwanajeshi wa 135 wa Kikanada kufa nchini Afghanistan.

Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads