Gerimani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Gerimani ni elementi yenye namba atomia 32 kwenye jedwali la elementi, uzani atomia ni 72,630. Alama yake ni Ge.
Remove ads
Tabia
Gerimani ni dutu mango na katika mazingira ya kawaida ni metali ngumu yenye rangi ya kifedha-nyeupe. Kiwango chake cha kuyeyuka ni 938.3 C°.
Ilitambuliwa mwaka 1886 na Mjerumani Clemens Winkler aliyebuni jina kwa heshima ya nchi yake ya kuzaliwa (lat. Germania)
Upatikanaji
Hupatikana mahali pengi ndani ya madini ya shaba na zinki kwa asilimia ndogo haitokei kiasili kama elementi tupu. Huchimbwa hasa China, Urusi, Kanada, Ufini na Marekani. Uzalishaji kwenye mwaka 2011 ilikuwa mnamo tani 100. Takriban theluthi moja ya uzalishaji wake ni kwa njia ya kurejeleza.[1].
Matumizi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads