Gervas Kasiga
Muigizaji na mtayarishaji filamu wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Gervas A. Kasiga (anafahamika zaidi kama Chuma au Junior[1]; alizaliwa 4 Februari 1982) ni mwigizaji wa filamu, mwandishi wa miswada ya filamu, mshairi, mwongozaji wa filamu na mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu kutoka nchini Tanzania.[2][3]
Anafahamika kwa kuongoza filamu maarufu ya "Fake Pastors (2007)" na kuongoza uchaguzi wa waigizaji wa filamu ya Bongoland II.
Ameandika miswada kadhaa ya Michezo ya Kuigiza ya Runinga (Tamthilia) kama vile "Gharika" na "Dira", miswada ya filamu maarufu za Unfortunate Love, Ripple of Tears, Village Pastor, Wende na nyinginezo.
Mwaka 2011 filamu yake fupi ya Wende ilichaguliwa kuoneshwa katika Tamasha la Sita la Filamu la Kimataifa la Kenya (KIFF). Vilevile amepata kuwa balozi wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (ZIFF) akiwakilisha wanafilamu wa ki-Tanzania.
Kasiga ameshafanya kazi mbalimbali za kisanaa na mashirika kama AMREF, PATHFINDER, THE NATURE AND CONSERVANCY, The International Theatre and Literacy Project (ITLP), CRDB - TANZANIA, College of Mathematics and Natural Science - University of Dodoma, Vocation Training Centre of Tanzania (VETA), Regina University - Canada na mengine mengi.[4] Ameshaendesha mafunzo mbalimbali ya uigizaji, uandishi wa miswada ya filamu, uchukuaji picha za video pamoja uongozaji katika mikoa ya Mwanza, Kigoma, Dodoma na Dar es salaam. Mafunzo hayo amekuwa akiyafanya aidha kupitia taasisi yake ya Dodoma Arts Center (DAC) au kupitia kampuni yake ya Bona Fide Films ama kwa kushirikiana na mashirika ya ndani na ya kimataifa.
Msanii huyu pia ni Mhadhiri Mwandamizi wa masomo ya Fasihi na Filamu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma - Tanzania. Vilevile ni Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)[5] nchini Tanzania.
Halikadhalika ni mwanablogu, anaendesha blogu ya Sebuleni. Gervas Kasiga katika seti ya Bongoland II[6][7]
Remove ads
Filmografia
Remove ads
Mashairi
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads