Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (kwa Kiingereza: Zanzibar International Film Festival, kifupi: ZIFF, pia hujulikana kama Festival of the Dhow Countries) ni tamasha la kila mwaka la filamu linalofanyika Zanzibar, Tanzania. Imeelezwa kuwa tukio kubwa zaidi la kitamaduni katika eneo la ukanda wa Afrika ya Mashariki. ZIFF ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa mwaka wa 1997 ili kuendeleza na kukuza tasnia ya filamu na mambo mengine ya kiutamaduni kama kichocheo cha ukuaji wa kijamii na kiuchumi wa kikanda.[1]
Remove ads
Tamasha la Filamu
Tamasha la kila mwaka la sanaa na tamaduni mbalimbali ni shughuli kuu ya ZIFF; tamasha hilo huadhimisha sanaa na tamaduni za bara la Afrika, Nchi za Ghuba, Iran, India, Pakistani na visiwa vya Bahari ya Hindi, kwa pamoja hujulikana kwa jina la nchi za Dhow. Sehemu kuu ya tamasha ni programu ya filamu inayojumuisha maonyesho ya ushindani na yasiyo ya ushindani. Filamu na video mbalimbali hushindania tuzo.[2]
Ingawa filamu za ushindani ni ambazo uzalishaji wake unahusiana na nchi za Dhow tu, programu ya tamasha inajumuisha filamu na video kutoka duniani kote zinazozungumzia mada zinazoakisi mambo ya ndani ya nchi za Dhow. [3]Shughuli na matukio ya tamasha hili ni pamoja na makongamano, warsha, na maonyesho ya filamu bora zaidi za ndani na kimataifa. Tamasha kubwa la muziki pia hufanyika likishirikisha wasanii kutoka Tanzania pamoja na wanamuziki wa kimataifa.[4] Programu ya tamasha pia hujumuisha vipengele maalum, warsha na semina kuhusu jukumu la filamu katika jamii za vijijini, masuala ya wanawake pamoja na watoto na maendeleo ya vijana. [5]
Tamasha hili bila shaka ndilo tamasha kubwa zaidi la sanaa na utamaduni barani Afrika, na linaendelea kuongoza kama tukio linalovutia watalii katika eneo hili. ZIFF sasa inatoa Tuzo 12 za Kimataifa zinazotolewa na majaji 5 wa Kimataifa. Kila mwaka ZIFF huonyesha zaidi ya filamu 150 zinazotengenezwa Afrika, Mashariki ya Kati, Ulaya, Amerika Kusini, Marekani na Asia.[6]

Tamasha la ZIFF sasa linaendesha programu 15 katika siku 10 zinazojumuisha:
- Film Competition
- Film Workshops
- Opening and Closing Nights
- Film Outreach Projections
- Women panorama
- Children panorama
- Village panorama
- Festival of Festivals
- Soko Film
- Art and Exhibition
- Children Film panorama
- UNICEF Life skills Camps
- Children Peace camps
- Difficult Dialogues
- Historical and Cultural Village Tours[7]
Matukio hayo mengi hufanyika katika eneo la Ngome Kongwe na Bustani za Forodhani na huwa bure kwa umma.[8] [9]
Remove ads
Tuzo
- Golden Dhow
- Silver Dhow
- Documentary
- Short/Animation
- East Africa Talent
- ZIFF Jury Award
- UNICEF Award
- ZIFF Life Time Achievement Award
- ZIFF Chairman Award
- Sembene Ousmane Award
- Signis Award
- East Africa Region Talent
- Signis Jury Award — Commendation
- Verona Award
Washindi wa Golden Dhow
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads