Ghuba ya Hudson

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ghuba ya Hudson
Remove ads

Ghuba ya Hudson (ing.: Hudson Bay, far.: baie d'Hudson, Kiinuktitut: Kangiqsualuk ilua) ni ghuba kubwa ya Bahari Atlantiki (Bahari ya Labrador) ndani ya ardhi ya Kanada mashariki. Eneo lake ni 819,000 km² (ni kubwa kuliko nchi ya Zambia). Ina umbo kama ziwa la ndani ya nchi kavu ikiunganishwa na bahari ya Labrador kwa njia nyembamba ya mlango wa Hudson yenye upana wa kilomita 64. Kuna mlango mdogo wa pili huu ni mlango wa Fury na Hecla.

Thumb
Ramani ya ghuba ya Hudson

Pwani zakle zinapaka na majimbo ya Nunavut, Manitoba, Ontario na Quebec.

Ghuba imepokea jina lake kutokana na mpelelezi Mwingereza Henry Hudson aliyekuwa mzungu wa kwanza kufika hapa mwaka 1610 kwa meli yake Discovery.

Remove ads

Viungo vya Nje

Britannica Online-Hudson Bay

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads