Eneo la Pibor
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Eneo la Pibor ni eneo maalumu la kiutawala nchini Sudan Kusini. [1] Lilimegwa na Jimbo la Jonglei.

Historia
Tangu mwanzo wa uhuru wa Sudan Kusini, watu wa Anyuak, Jie, Kachepo, na Murle huko Jonglei walitafuta uhuru zaidi kutoka kwa serikali ya Jimbo la Jonglei lililotawaliwa na Wanuer na Wadinka. Uasi ulitokea kwa kutumia silaha dhidi ya Serikali ya Sudan Kusini.
Mazungumzo ya amani katika mwaka wa 2014 yalileta maafikiano ambayo yaliunganisha maeneo mawili ya Pibor na Pochalla ndani ya jimbo la Jonglei kuwa eneo jipya la kiutawala la Greater Pibor (GPAA) linalojiendesha yenyewe. [2]
Kati ya miaka 2015 hadi 2020 eneo hilo maalum la utawala lilikuwa Jimbo la Boma [3] [4] [5] lakini tangu kurudishwa kwa majimbo 10 ya kiasili limekuwa tena eneo maalum la kiutawala lililopo moja kwa moja chini ya serikali kuu.[6]
Remove ads
Miji
Makao makuu ya eneo hilo ni Pibor. Idadi ya wakazi wa mji wa Pibor ilikadiriwa kuwa chini ya watu 1,000 kwenye mwaka wa 2005.
Mji wa Pochalla katika wilaya ya Pochalla uko moja kwa moja kwenye mpaka wa Ethiopia. Mji uko takriban kilomita 470 kutoka Juba kupitia barabara.
Wakuu wa eneo
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads