Grenada

From Wikipedia, the free encyclopedia

Grenada
Remove ads

Grenada ni nchi ya kisiwani kusini mwa Bahari ya Karibi. Iko kaskazini kwa Trinidad na Tobago na kusini kwa Saint Vincent.

Ukweli wa haraka


Ni nchi mwanachama wa jumuiya ya madola na mkuu wa Dola ni Mfalme Charles III wa Uingereza anayewakilishwa kisiwani na Gavana Mkuu.

Remove ads

Jiografia

Eneo la nchi ni kisiwa kikuu cha Grenada pamoja na visiwa kadhaa za funguvisiwa ya Grenadini kama vile Carriacou, Petit Martinique, Rhonde Island na vingine vidogo.

Idadi kubwa ya wakazi iko Grenada penyewe pamoja na miji ya St. George's (mji mkuu), Grenville na Gouyave.

Visiwa vyote ni vya asili ya kivolkeno vyenye ardhi yenye rutuba. Grenada ina milima, na mkubwa zaidi ni mlima St. Catherine wenye kimo cha mita 840.

Remove ads

Watu

Wakazi ni 110,000: walio wengi (82%) ni wa asili ya Afrika wametokana na watumwa waliopelekwa huko kulima mashamba ya miwa au ni machotara (13%) waliotokana na watumwa wale na mabwana wao Wafaransa. Waliobaki (5%) ni Wazungu na Wahindi. Wananchi walio wengi wanaishi nje: ni kama mara mbili kuliko waliobaki nchini.

Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini walio wengi kwa kawaida wanaongea Krioli.

Upande wa dini, karibu wote ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (53%). Kati ya madhehebu ya Uprotestanti, wanaongoza Waanglikana.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads