Chotara

From Wikipedia, the free encyclopedia

Chotara
Remove ads

Chotara (kutoka Kihindi; pia: suriama kutoka Kiarabu na shombe) ni kiumbe hai ambacho kimetokana na makabila zaidi ya moja ya spishi yake. Kwa mfano, binadamu ambaye alizaliwa na baba Mzungu na mama Mwafrika anaitwa hivyo.[1]

Thumb
Familia pana ya kichotara ya Afrika Kusini ikionyesha tofauti katika rangi ya ngozi na nyinginezo.
Thumb
Barack Obama, rais wa Marekani (2008-2016) ni chotara, kwa sababu baba yake alikuwa Mjaluo wa Kenya na mama alikuwa Mmarekani mwenye asili ya Ulaya.

Katika lugha mbalimbali kuna majina maalumu kwa aina za machotara: kwa mfano katika Kihispania kuna Mulato, zambo na mestizo; katika Kireno kuna mulato, caboclo, cafuzo, ainoko na mestiço.

Pengine sensa zinauliza asili ya wakazi, zikiacha nafasi ya kutaja asili zaidi ya moja.

Kundi la pekee ni Machotara wa Afrika Kusini waliotokana na mchanganyiko wa Wazungu, Waafrika na Wamalay na kutengwa chini ya sheria ya apartheid nchini Afrika Kusini.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads