Himo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Himomap

3.38°S 37.55°E / -3.38; 37.55

Thumb
Picha ya Himo kwa macho ya ndege

Himo ni mji mdogo katika Wilaya ya Moshi Vijijini ya Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.[1]

Himo huhesabiwa bado kama sehemu ya kata ya Makuyuni.

Himo iko kwenye njiapanda ya barabara T2 (Chalinze-Arusha) na T15 (Himo-Taveta). Umbali wake na Moshi ni km 29, hadi mpakani mwa Taveta ni km 15. Himo ndipo inaanza barabara ya Marangu ambayo ni sehemu ya kuanza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro.

Ilianza kukua wakati wa kufungwa kwa mpaka baina ya Kenya na Tanzania katika miaka ya 1980 ikiwa kitovu cha biashara ya magendo.[2]

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.