Mkoa wa Kilimanjaro

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mkoa wa Kilimanjaro
Remove ads

Mkoa wa Kilimanjaro ni mojawapo ya mikoa 31 ya Tanzania, uliopo kaskazini-mashariki mwa nchi. Unapakana na Kenya upande wa kaskazini, Mkoa wa Arusha magharibi, na Mkoa wa Tanga upande wa kusini. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022, mkoa una wakazi 1,861,934. Makao makuu ya mkoa huo yako Moshi mjini. Mkoa huo unajulikana zaidi kwa kuwa na Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika, ambao pia ni kivutio kikuu cha utalii kutoka dunia nzima. Mkoa huu una historia tajiri ya biashara, na kilimo, hasa cha kahawa, na unajulikana kwa kiwango cha juu cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi ukilinganisha na mikoa mingine ya Tanzania, ingawa teknolojia ya utandawazi katika eneo kubwa haijashamiri.

Ukweli wa haraka Nchi, Wilaya ...
Remove ads

Wakazi

Mkoani Kilimanjaro kuna wakazi wapatao 1,861,934 (sensa ya mwaka 2022[1].).

Makabila makubwa mkoani humo ni Wachagga, Wagweno na Wapare, ambapo pia kuna makabila mengine madogomadogo kama Wamasai na Wakamba.

Wilaya

Mkoa wa Kilimanjaro una wilaya 7 ambazo ni: Hai, Mwanga, Moshi mjini, Moshi vijijini, Rombo na Same na ile mpya ya Siha.

Maelezo zaidi Ramani, Wilaya au manisipaa ...
Remove ads

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2020 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

  • Hai (Saashisha Mafuwe)
  • Siha (Dr Godwin Mollel)
  • Moshi Mjini (Priscus Tarimo)
  • Mwanga
  • Same Mashiriki
  • Same Magharibi
  • Moshi Vijijini (Prof. Patrick Ndakidemi)
  • Vunjo (Dr Charles Kimei)
  • Rombo (Prof. Adolf Mkenda)

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads