Historia ya awali
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Historia ya awali (kwa Kiingereza: prehistory) ni kipindi kirefu sana cha historia, kikichukua miaka yote tangu binadamu walipotokea duniani mpaka historia andishi ilipoanza (huko Mesopotamia miaka 3,300 hivi KK).[1]

Ingawa muda ni mrefu sana na ni wa msingi kwa historia yote iliyofuata, watu hawakuwa wengi kama walivyozidi kuwa kadiri ya maendeleo yao. Maisha yao hayakuwa marefu kutokana na ugumu wa mazingira na utovu wa vifaa na dawa mbalimbali.
Remove ads
Jina
Katika lugha nyingi msamiati ni kabla ya historia (k.mf. kwa Kiingereza ni pre-history), ambao unatokana na maneno ya Kigiriki προ, pro, yaani "kabla" na ιστορία, istoria, yaani "historia").
Paul Tournal mwanzoni alitunga neno la Kifaransa “Pré-historique” katika kuelezea ugunduzi aliofanya katika mapango ya kusini mwa Ufaransa.
Neno hilo lilitumika katika Ufaransa kuanzia miaka ya 1830 kuelezea kipindi kabla ya uandishi, na baadaye likaingizwa na Daniel Wilson katika Kiingereza mwaka 1851.
Remove ads
Vipindi vya historia ya awali
Sehemu kubwa kabisa ya historia ya binadamu ilitokea kabla ya maandishi kugunduliwa. Kuhusu zamani hizo tunapata habari kutokana na utafiti wa akiolojia.
Kwa njia hiyo tunakuta mabaki ya ya siku zile kama vile vifaa, majengo au pia uchoraji kwenye kuta za mapango lakini tunakosa maelezo jinsi yanavyopatikana tangu watu waanze kuandika kumbukumbu.
Kati ya vipindi vya historia ya awali ni zama za mawe. Wakati huo wote watu walipiga hatua muhimu ya maendeleo, kama vile kubuni vifaa vya kwanza, kilimo, na kujenga vijiji na miji ya kwanza.
Hata vyanzo vya teknolojia za metali, kama zama za shaba na zama za chuma, vilitokea kabla ya kugundua maandishi katika sehemu nyingi za dunia.
Lakini mifano ya kwanza ya utamaduni wa kimaandishi ilitokea wakati wa kubuni matumizi ya shaba na bronzi huko Misri na Mesopotamia.
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads