Kucha (Hyliota)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kucha (Hyliota)
Remove ads

Kucha wa jenasi Hyliota ni ndege wadogo ambao zamani waliainishwa katika Sylviidae, familia ya kucha wengine. Sasa wataalamu wanakubaliana kwamba ndege hawa hawana mnasaba na Sylviidae. Labda wana mnasaba na familia Promeropidae (ndegesukari wa Afrika Kusini). Hadhi yao haijaamua bado lakini wapewa familia yao kwa sasa: Hyliotidae. Wanafanana na tatata. Kucha hawa wana rangi ya nyeusi au zambarau mgongoni na nyeupe, machungwa au njano chini. Hula wadudu na pengine beri na mbegu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe ndani ya uoto mzito. Jike huyataga mayai 2-5.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi za Afrika

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads