Ibrahim Hamad
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ibrahim Abdallah Hamad (maarufu kwa jina la Ibrahim Bacca,[1]; alizaliwa 12 Novemba 1997) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutokea nchini Tanzania anayecheza nafasi ya mlinzi wa kati kwenye klabu ya Young Africans S.C.. Anazichezea pia timu za taifa za Zanzibar na Tanzania.
Kazi
Hamad alianza kucheza soka la kulipwa mwaka 2017 katika klabu ya Jang'ombe Boys F.C. inayoshiriki Ligi kuu ya Zanzibar. Alihamia Malindi S.C. mwaka 2019 na kucheza misimu miwili. Mwaka 2021, alihamia KMKM F.C. ambako alishinda taji la Ligi Kuu ya Zanzibar msimu wa 2021–22. Mnamo 14 Januari 2022 alihamia klabu ya Young Africans inayoshiriki NBC Premier League ambapo alishinda mataji ya ligi mara mbili mfululizo, Taji moja la Mashindano ya FA na Taji moja la Ngao ya Hisani.[2][3] Mnamo Novemba 2023 aliongeza mkataba wake mpaka mwaka 2027, baada ya kiwango cha hali ya juu alichokionyesha dhidi ya Al Ahly kwenye Mashindano ya Klabu bingwa Afrika, siku maalumu ilitengwa kwa ajili ya kumuenzi na kupewa jina la "Bacca Day".[4]
Remove ads
Kimataifa
Hamad alitajwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar kwenye mashindano ya CECAFA mwaka 2017, ambapo timu yake ilimaliza nafasi ya pili.[5]
Mnamo tarehe 24 Machi 2023, alitajwa kwa mara ya kwanza kwenye kisosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kenye mchezo dhidi ya Uganda katika mashindano ya kufuzu fainali za AFCON za mwaka 2023 ambapo walishinda goli 1 – 0.[6] Alikua katika kikosi cha mwisho kilichoiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya AFCON yam waka 2023.[7]
Remove ads
Maisha binafsi
Hamad ni Muislamu mcha Mungu. Rafiki yake wa karibu alifariki katika ajali ya MV Spice Islander I mwaka 2011. Akiwa kijana, Hamad alifanya kazi ya kumenya viazi ili kuwathibitishia wazazi wake kwamba anaweza kufanya kazi. Alishawahi kuwa kwenye kikosi cha kuzuia magendo cha Zanzibar.[1]
Mataji
- KMKM
- Ligi Kuu Ya Zanzibar: 2021–22
- Young Africans
- Ligi Kuu Tanzania Bara: 2021–22, 2022–23
- Kombe la FA Tanzania: 2021–22
- Ngao ya Jamii Tanzania: 2022
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads