Ice Prince

Rapa wa Nigeria From Wikipedia, the free encyclopedia

Ice Prince
Remove ads

Panshak Henry Zamani(anajulikana zaidi kama Ice Prince Zamani au Ice Prince, alizaliwa 30 Oktoba 1986) ni rapper, mwimbaji na mtunzi wa nyimbo wa Nigeria.[1] Alipata umaarufu baada ya kuachia wimbo wake "Oleku", ambao umekuwa moja ya nyimbo zilizofanyiwa remix nyingi zaidi nchini Nigeria. Alishinda Hennessy Artistry Club Tour mwaka 2009. Albamu yake ya kwanza ya studio "Everybody Loves Ice Prince" ilitolewa mwaka 2011, ikiwa na nyimbo maarufu kama "Oleku", "Superstar", na "Juju".[2][3] Mwaka 2013, Ice Prince alitoa albamu yake ya pili ya studio, "Fire of Zamani", ambayo ilijumuisha nyimbo kama "Aboki", "More", "Gimme Dat", na "I Swear". Mnamo Julai 1, 2015, alitangazwa kuwa makamu wa rais wa Chocolate City na alishikilia nafasi hiyo hadi alipoondoka kwenye lebo hiyo mwaka 2016.[4][5] Amefanya kazi na marapa mashuhuri barani Afrika kama Navio wa Uganda, Khaligraph Jones wa Kenya, AKA wa Afrika Kusini, na Sarkodie wa Ghana miongoni mwa wengine.

Thumb
Ice Prince
Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads