Uganda

nchi ya Afrika Mashariki ya Kati From Wikipedia, the free encyclopedia

Uganda
Remove ads

Uganda,rasmi Jamhuri ya Uganda ni nchi ya isiyo na pwani katika Afrika ya Mashariki. Imepakana na Kenya upande wa mashariki, Sudan Kusini upande wa kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi, Rwanda na Tanzania upande wa kusini.Mnamo 2024 ina idadi ya watu takriban Milioni 46 na kuwa nchi ya 31 duniani kwa ukubwa wa idadi ya watu na ina eneo la kilomita za mraba 241,038. Kampala ndio mji mkuu na jiji kubwa la Uganda

Ukweli wa haraka Jamhuri ya Uganda Lipabuliika ya Uganda (Luganda) Republic of Uganda (Kiingereza), Mji mkuu na mkubwa ...

Uganda ni jamhuri ya urais yenye mfumo wa vyama vingi vya siasa. Ilipata uhuru kutoka Uingereza mwaka 1962 na tangu wakati huo imepitia vipindi vya hali ya kisiasa isiyo thabiti, ikiwemo tawala za kijeshi. Hata hivyo, katika miongo ya hivi karibuni, Uganda imepata utulivu wa kisiasa kwa kiasi fulani na mageuzi ya kiuchumi, ingawa changamoto zinazohusiana na utawala na haki za binadamu bado zipo.

Uchumi wa Uganda unategemea zaidi kilimo, ambacho kinawaajiri watu wengi. Nchi pia imekuwa ikishuhudia ukuaji katika sekta kama huduma, viwanda, na utafutaji wa mafuta. Inajulikana kama "Lulu ya Afrika" kutokana na utofauti mkubwa wa viumbe hai, Uganda ni makazi ya wanyama mbalimbali, wakiwemo sokwe milimani walioko hatarini kutoweka, na ina maeneo ya asili maarufu kama vile Ziwa Viktoria, Mto Nile, na Milima ya Rwenzori.

Remove ads

Jina

Jina Uganda lina asili yake katika ufalme wa Buganda ulioko kusini mwa nchi pamoja na mji mkuu, Kampala.

Thumb
Ramani ya Uganda

Jiografia

Tazama piaː Orodha ya milima ya Uganda; Orodha ya maziwa ya Uganda; Orodha ya visiwa vya Uganda; Wilaya za Uganda

Uso wa nchi umepata tabia yake kutokana na maziwa makubwa, mito, milima ya juu na tambarare.

Upande wa kusini nchi imepakana na Ziwa Nyanza Viktoria ambalo kwa eneo ndilo ziwa kubwa kuliko yote ya Afrika. Maziwa makubwa mengine upande wa magharibi ni Ziwa Albert na Ziwa Edward.

Mto mkubwa ni Nile inayopita nchi yote kati ya Ziwa Viktoria hadi Ziwa Albert na kuendelea hadi mpaka wa Sudani ikiitwa mwanzoni Nile ya Viktoria na baadaye Nile ya Albert.

Milima ya Ruwenzori ni kati ya milima mikubwa kabisa ya Afrika baada ya Kilimanjaro na Mlima Kenya.

Kusini kuna ardhi yenye rutuba na kilimo kinastawi vizuri.

Remove ads

Historia

Makala kuu: Historia ya Uganda

Historia ya kale

Eneo la Uganda limeona uhamiaji wa vikundi vingi waliowazidi wenyeji asili (walioishi huko tangu miaka 50,000 kama si 100,000 KK).

Kusini liliingiliwa hasa na wakulima Wabantu. Kaskazini iliona kufika kwa Waniloti kwa mfano Waluo na baadaye Karimojong.

Tangu karne ya 15 himaya mbalimbali zilianza kujengwa na kati ya hizo ni hasa falme za Buganda, Ankole, Bunyoro Toro zilizoendelea kuwa muhimu hadi kuja kwa ukoloni na kwa kiasi fulani kama urithi wa kiutamaduni hata katika Uganda ya kisasa.

Ukoloni

Karne ya 19 iliona kufika kwanza kwa Waarabu na baadaye kwa Wazungu. Kila mmoja alileta dini yake yaani Uislamu na Ukristo wa Kikatoliki na wa Kianglikana.

Katika mashindano juu ya Afrika ya Kati Waingereza walifaulu katika kushindana na Waarabu, Wafaransa na Wajerumani. Walienea kwa mapatano na Buganda wakisaidiana kukomesha upinzani kutoka falme za jirani.

Baadaye Waingereza walikuwa na nguvu ya kutosha kuamua hata mambo ya ndani ya Buganda wakatangaza Uganda wote kuwa nchi lindwa tangu mwaka 1894.

Baada ya uhuru

Uganda ilipata uhuru wake tarehe 9 Oktoba 1962 kwa katiba ya jamhuri yenye serikali ya kibunge.

Rais wa kwanza alikuwa Kabaka Sir Edward Mutesa II na waziri mkuu Milton Obote.

Mwaka 1967 Obote alibadilisha katiba akamfukuza Kabaka nchini.

Serikali ya Obote ilipinduliwa na mkuu wa jeshi Idi Amini mwaka 1971. Utawala wake ulikuwa kipindi cha udikteta ulioharibu uchumi wa nchi na misingi ya dola. Takriban watu 300,000 waliuawa chini ya Amin ama wapinzani wa siasa yake ama watu wa makabila yaliyotazamwa kuwa maadui wa serikali. Raia wenye asili ya Asia walifukuzwa katika nchi na mali yao yote kutwaliwa na serikali.

Mwaka 1978 vikosi vya jeshi la Uganda viliingia Tanzania na kuvamia maeneo ya mpakani kaskazini kwa mto Kagera. Mwaka 1979 Tanzania ilijibu kwa njia ya vita na jeshi lake pamoja na wapinzani wa Uganda walishinda jeshi la Amin na kumfukuza dikteta nchini. Rais wa baadaye Yoweri Museveni alikuwako kati ya wanamgambo waliosaidiana na Watanzania.

Uchaguzi wa mwaka 1980 ulimrudisha madarakani Milton Obote aliyeanzisha upya udikteta na kuua watu ovyo. Wapinzani wake wakiongozwa na Museveni walirudi porini wakashika silaha. Katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kundi la Museveni likashinda na kutwaa serikali tangu mwaka 1986.

Museveni alichaguliwa rais katika kura bila vyama vya upinzani za 1996 na 2001.

Mwaka 2005 ulikuwa na uchaguzi wa vyama vingi wa kwanza. Museveni alipata kibali cha bunge kwa badiliko la katiba lililomruhusu kugombea urais tena mwaka 2006 akachaguliwa mara ya tatu.


Remove ads

Demografia

Thumb
Ramani ya Uganda ikionyesha makabila na lugha.

Wakazi wa Uganda wameongezeka kutoka 9,500,000 (1969) hadi 34,634,650 (2014), hivyo wengi wao ni vijana kuliko nchi zote duniani. Umri wa wastani ni miaka 15 tu.

Kabila/Asili

Makabila makubwa ni Waganda (16.9%), Wanyankole (8.5%), Wanyoro (7.7%), Wasoga (7.4%), Walangi (7.1%), Wakiga (6.9%), Wateso (6.4%), Waacholi (5.7%), Wagisu (4.6%), Walugbara (4.2%). Wengineo ni 33.6%.

Lugha

Nchini kuna lugha asilia 40 hivi, ambazo zinagawanyika katika makundi makubwa mawili: lugha za Kibantu upande wa kusini na lugha za Kinilo-Sahara upande wa kaskazini. Pia kuna lugha za Kisudani na lugha za Kikuliak. Hata hivyo lugha rasmi ni Kiingereza na Kiswahili.

Dini

Upande wa dini, kadiri ya sensa ya mwaka 2014, 84.5% za wakazi wanafuata Ukristo, hasa katika madhehebu ya Kikatoliki (39.3%) na ya Kianglikana (32%), halafu Wapentekoste (11.1%) na mengineyo. Waislamu ni 13.7%, wengi wao wakiwa Wasuni. Wanaoendelea kufuata dini asilia za Kiafrika ni 0.1% tu.

Miji ya Uganda

Remove ads

Tanbihi

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads