Ida Ljungqvist
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ida Ljungqvist (alizaliwa tarehe 27 Septemba 1981) ni Mtanzania-Mswidi na ni mwanamitindo wa Kiafrika wa kwanza kuchaguliwa kama playboy playmate wa mwezi na ni wa 50 kwa maplaymate wa mwaka.
Maisha yake ya awali
Ljungqvist alizaliwa Tanzania, mama yake ni Mtanzania wakati baba yake ni raia wa Uswidi [1]. Kutokana na baba yake kufanya kazi katika UNICEF Ljungqvist alinufaika kuweza kuongea lugha za Kiingereza, Kiswahili na Kiswidi. Ljungqvist ana shahada ya mitindo na Masoko.
Familia
Mwaka 2007 alifunga ndoa na Joshua R. Lang. Baada ya miaka mitano walitalakiana.
Kazi
Mwaka 2007 Ljungqvist alitambuliwa na aliyekuwa playmate wa mwaka Sara Jean Underwood. [2][3] Machi 2008 alitajwa kama playboy wa playmate wa mwezi na Playmate wa mwaka 2009. Na yeye ni mwanamitindo wa kiafrika wa kwanza na wa kiswidi wa pili kutajwa kama playmate wa mwaka. [4]
Tangu awe playmate wa mwaka Ljungqvist amejikita kwenye kazi za Uwezeshaji, teknolojia ya uendelezaji wa kimataifa pamoja na kuongeza ufahamu juu ya shirika na kukusanya fedha.
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads