Mwanamitindo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mwanamitindo ni mtu mwenye kazi ya mkao, au kuonesha kazi za sanaa au maonyesho ya mavazi, kwa kawaida hutafuta soko kwa ajili ya bidhaa. Mara kwa mara hutumiwa kwenye matangazo ya televisheni na vyombo vya habari vya uchapishaji, kwa mfano magazeti na majarida[1].


Aina za wanamitindo
Kuna aina chungumzima za wanamitindo. Baadhi yao hutumia sehemu fulani tu za miili yao. Kwa mfano, mwanamitindo wa mkono ni mtu ambaye hutumia mikono yake tu kufanyia shughuli za kiuanamitindo. Mwanamitindo wa mkono hutumika kuoneshea bidhaa fulani, kwa mfano pete au saa. Wanamitindo wa aina hii kawaida hutumiwa kwa ajili ya matangazo tu, basi. Msanii Marc Engelhard hufanya sehemu za mwili wake zipatikane kwa picha hiyo.[2]
Wanamitindo wa fasheni hutumiwa kwa kuuza mavazi au vipodozi. Watu wanaotengeneza nguo hutumia wanamitindo wa mavazi kuvaa nguo zao na kuoneshea kwenye maonyesho ya mavazi. Wanamitindo hao watatembea juu na chini wakionesha mavazi yao sakafuni panapoitwa en:catwalk au runway kuonyesha nguo hizo kwa watu wengine.[3]
Wanamitindo wa sanaa hukodishwa na wapiga picha, wachoraji na wasanii wengine kwa ajili ya mkao ili kutengeneza sanaa zao.
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.