Ishmaeli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ishmaeli (au Ismaili, kwa Kiebrania יִשְׁמָעֵאל, Yišmāʻēl: kwa Kiarabu إسماعيلʾ, Ismāʿīl) alikuwa mtoto wa kwanza wa Abrahamu (au Ibrahimu) na Hagari (au Hajiri) kadiri ya Biblia [1]na ya Kurani.

Ishmaeli katika Biblia
Mungu alikuwa amemuahidia Abrahamu uzao mkubwa kama nyota za mbinguni, naye akaamini ingawa alikuwa hajapata hata mtoto mmoja: ndiyo imani iliyompendeza sana Mungu (Mwa 15:1-6).
Lakini Abrahamu alizidi kuzeeka pamoja na Sara bila ya kuzaa watoto. Baada ya kusubiri muda mrefu mno Sara akamwambia azaliane na Hagari aliye mtumishi wa kike. Mwana huyu wa Hagar akaitwa Ishmaeli (Mwa 16:1-15). Lakini baadaye kukawa na fitina kati ya Sara na Hagari hivyo huyo akafukuzwa pamoja na mtoto, baada ya Sara pia akashika mimba na kumzaa mtoto Isaka.
Mwa 21:1-21 inatusimulia jinsi Mungu alivyotimiza ahadi yake kwa kumjalia Sara amzalie Abrahamu mtoto huyo katika uzee na utasa. Isaka ni mtoto wa imani, si wa mwili, naye ni huru, tofauti na Ishmaeli mtoto wa mtumwa ambaye hastahili kurithi pamoja na mdogo wake. Isaka, baba wa Israeli alipata baraka kuu, naye ni mfano wetu watu wa Agano Jipya. Ishmaeli alibarikiwa pia kwa ajili ya baba yake, naye ni mfano wa Agano la Kale ambapo watu wanategemea mambo ya kimwili (kutahiriwa, kunawa, kubagua vyakula n.k.) na hivyo ni watumwa (Gal 4:21-5:1).
Kadiri ya kitabu cha Mwanzo alishiriki pamoja na mdogo wake Isaka mazishi ya baba yake akafariki akiwa na umri wa miaka 137.[2]
Ishmaeli alizaa watoto wa kiume 12 ambao wanahesabiwa mwanzo wa Waarabu, hasa wale wa Kaskazini.
Remove ads
Ishmaeli katika Uislamu

Ishmaeli anahesabiwa nabii muhimu na babu wa Muhammad, mwanzilishi wa dini ya Uislamu.
Ingawa Kurani haitaji jina la mtoto ambaye Abrahamu alikuwa tayari kumchinjia Mungu, wanazuoni walifikia makubaliano kwamba alikuwa Ishmaeli, si Isaka.
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads