James Harden

Mchezaji wa mpira wa kikapu kutoka marekani From Wikipedia, the free encyclopedia

James Harden
Remove ads

James Edward Harden (alizaliwa 26 Agosti 1989) ni mchezaji wa mpira wa kikapu kutokea Marekani anayeichezea timu ya Houston Rockets katika Chama cha taifa cha mpira wa kikapu (NBA).

Thumb
James Harden akiwa anachezea timu ya kikapu ya Houston Rockets mwaka 2016.

James alicheza mashindano ya mpira wa kikapu akiwa chuoni na chuo cha Arizona State. Mwaka 2009, Kawhi alichaguliwa kama chaguo namba tatu katika machaguzi ya wachezaji wa wadogo katika Chama cha taifa cha mpira wa kikapu(NBA) nchini Marekani katika timu ya Oklohoma City Thunder. Mwaka 2012, aliisaidia timu yake kufika fainali ya mashindano ya Chama cha taifa cha mpira wa kikapu (NBA) lakini walishindwa kuifunga timu ya Miami Heat waliyokua wakipambana nayo.

Mnamo mwaka msimu wa 2012-2013 wa Chama cha taifa cha mpira wa kikapu (NBA), Harden aliuzwa kuelekea timu ya Houston Rockets. Wakati akiwa anaichezea timu ya Houston Rockets alifanikiwa kua mfungaji bora na alipata kujulikana sana kama mchezaji mzuri [1][2] na pia kama mmoja kati ya wachezaji wakubwa kwenye ligi. [3]

Harden amefanikiwa kuteuliwa katika timu ya mastaa marekani kwa mara tatu. Harden ameweza kuchezea timu ya wanaume ya mpira wa kikapu ya nchini Marekani mara mbili, kushinda medali mbili za dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka 2012 na mashindano ya kombe la Dunia ya FIBA mwaka 2014.

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads