Jerry Zucker

From Wikipedia, the free encyclopedia

Jerry Zucker
Remove ads

Jerry Zucker (amezaliwa tar. 11 Machi 1950) ni mwongozaji wa filamu kutoka nchini Marekani, anayejulikana sana kwa kuongoza filamu za vichekesho, na filamu bab-kubwa ya Ghost.

Ukweli wa haraka Amezaliwa, Kazi yake ...

Zucker alizaliwa mjini Milwaukee, Wisconsin, akiwa kama mtoto wa Charlotte (amekufa 2007) na Burton Zucker, ambaye alikuwa mjenzi wa makazi ya kukodisha.[1] Alihitimu katika shule ya Shorewood High School.[2]

Kazi za awali za Zucker alianza na Jim Abrahams na ndugu yake David Zucker katika Kentucky Fried Theatre mjini Pico Blvd huko West Los Angeles ambamo walianza mtindo wao wa ucheshi wa hadhara moja kwa moja. Kuanzia hapo watatu wale waliendelea pamoja na baadaye wakashirikiana kuongoza filamu ya Airplane! mnamo 1980 na kisha wakaenda kufanya Top Secret! mnamo mwaka wa 1984, na Ruthless People mnamo mwaka wa 1986. Mnamo mwaka wa 1990, aliazima maarifa yake ya uongozaji katika igizo la Ghost, ambayo ilichaguliwa katika tuzo ya Academy Award ikiwa kama Picha Bora. Juhudi zake za hivi karibuni ni pamoja na filamu ya 2001 Rat Race (ambayo amejiunga tena na nyota wa filamu ya Ghost Whoopi Goldberg).

Kama jinsi alivyo ndugu yake David Zucker, Jerry mara kwa mara humshirikisha mama yaker, Charlotte (ambaye amekufa 2007), na dada'ke , Susan Breslau, katika vipande vidogo vya katika filamu zake. Kwa pamoja akiwa na Jim Abrahams, wakina Zuckers wakaanzisha kikosi cha waongozaji wa filamu "Zucker, Abrahams and Zucker au kifupi ZAZ".

Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads