Mwanza (mji)
jiji lililo karibu na ziwa From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Jiji la Mwanza ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Mwanza. Mji upo kando la ziwa Viktoria Nyanza Kulingana na sensa ya mwaka 2012 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 706,453 (ukijumlisha wakazi wa Wilaya ya Nyamagana na sehemu za Wilaya ya Ilemela).[2]: 173 Mwaka 2022 walihesabiwa 1,004,521 [3].

Jiji hili limekuwa na vivutio mbalimbali vikiwemo mawe yaliyo katika Ziwa Victoria katika eneo la Nyanza. Pia jirani kuna hifadhi za wanyama wa porini kama Sanane, ambapo kuna wanyama kama simba, swala, pundamilia, sokwe,duma na chui
Remove ads
Historia
Mwanza ilianzishwa na Wajerumani wakati wa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Mahali paliteuliwa kutokana na nafasi ya bandari asilia upande wa kusini ya Ziwa Viktoria. Wajerumani waliuita mji kwa jina "Muansa" inaaminiwa ilikuwa matamshi yao ya neno "nyanza". Walijenga boma kubwa iliyoendelea kitovu cha mji. Takwimu ya Kijerumani ya 1912 ilihesabu wazungu 85, Wagoa 15, Wahindi wengine 300 na Waarabu 70 lakini haikutaja wakazi Waafrika. Palikuwa na makampuni ya biashara 12 ya kizungu na 50 ya Wahindi.[4].
Remove ads
Picha
- Mwanza: Boma la Kijerumani mnamo 1912
- Mwanza: miamba ya Bismarck Rock
Tazama pia
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads