Mkoa wa Mwanza

Mkoa wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia

Mkoa wa Mwanza
Remove ads

Mkoa wa Mwanza ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Umepakana na Geita upande wa magharibi, Shinyanga na Simiyu upande wa kusini na Mara upande wa mashariki. Ziwa la Viktoria Nyanza liko kaskazini. Ni mkoa mdogo kwa eneo lake la km2 25,233, lakini wa pili kwa idadi ya watu kwa kuwa na wakazi 3,699,872 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 [1]. Makao makuu yako Mwanza mjini.

Ukweli wa haraka Nchi, Wilaya ...
Thumb
Mwanza

Mkoa una postikodi namba 33000.

Thumb
Mwamba wa Bismarck ziwani.
Remove ads

Wilaya

Kabla ya kumegwa na kuzaa mkoa mpya wa Geita, mkoa wa Mwanza ulikuwa na wakazi 2,942,148 (sensa ya mwaka 2002) katika wilaya 8 ukiwa na eneo la 19,592 km2.

Kwa sasa wilaya ni: Ukerewe, Magu, Sengerema, Buchosa, Misungwi, Kwimba, Nyamagana na Ilemela. Jiji la Mwanza ndani yake lina wilaya za Nyamagana na Ilemela.

Maelezo zaidi Ramani (kabla ya 2012), Wilaya au manisipaa ...
Remove ads

Wakazi

Makabila makubwa ya Mwanza ndio Wasukuma na Wazinza upande wa bara, halafu Wakerewe na Wakara visiwani.

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads