Joseph Bilczewski

From Wikipedia, the free encyclopedia

Joseph Bilczewski
Remove ads

Josef Bilczewski (26 Aprili 186020 Machi 1923) alikuwa askofu mkuu wa Lviv (leo nchini Ukraina) kuanzia mwaka 1900 hadi kifo chake, akijitahidi kwa upendo wenye ari kuinua maadili na ujuzi wa dini wa mapadri na waumini wa jumla wa jimbo lake la Kilatini[1][2][3]

Thumb
Picha halisi ya Mt. Józef Bilczewski.

Lakini pia alisaidia watu kwa kila namna wakati wote wa Vita vikuu vya kwanza, akajaribu kupatanisha Wapolandi na Waukraina waliochukiana na kupigana, akaendelea baada ya Wakomunisti kuteka nchi hizo mbili.[1][3]

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 26 Juni 2001 halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 23 Oktoba 2005.[2]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads