Julie Billiart
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Julie Billiart (Cuvilly, Ufaransa, 12 Julai 1751 — Namur, Ubelgiji, 8 Aprili 1816) alikuwa bikira aliyeanzisha kwa ajili ya malezi ya wasichana shirika la Masista wa Bibi Yetu wa Namur mwaka 1803[1].

Alikuwa maarufu kwa upendo wake wa pekee akaeneza kwa bidii ibada kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu[2].
Siku hizi masista wake ni 2,000 hivi, nao wanaishi katika nchi 20 za mabara matano, zikiwemo Kenya na Tanzania.
Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius X tarehe 13 Mei 1906 halafu mtakatifu na Papa Paulo VI tarehe 22 Juni 1969.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads