Just Stand Up!

From Wikipedia, the free encyclopedia

Just Stand Up!
Remove ads

"Just Stand Up!" ni wimbo ulioimbwa na mjumuisho wa wasanii mbalimbali, wanaoimba miondoko ya pop, R&B, rok, na Katri katika tamasha la kukusanya fedha kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa saratani.Mtayarishaji na mtunzi wa nyimbo wa Marekani L.A Reaid aliandaa ushirikiano huo wa wasanii baada ya kukutana na mwanzilishi wa tamasha la Pingana na Saratanai, na kuandaa tamasha litakalosaidia kuchangisha fedha kwa ajili ya kukuza mfuko huo. Waandaaji hawa waliandaa wimbo huu, kwa kushirikiana na waimbaji wa Kimarekani kama vile Bebyface na single hii ilitoka tarehe 21 Agasti 2008

Ukweli wa haraka Single ya Artists Stand Up To Cancer, Imetolewa ...

Waimbaji hawa waliimba wimbo huu moja kwa moja ambayo ilirushwa hewani katika vyombo vya habari mbalimbali kama vile ABC, CBS na NBC tarehe 5 Septemba 2008.[1][2] Single hii ilitolewa tena tarehe 30 septemba 2008, na pia ilitoka na nakala ya tamasha la moja kwa moja. Lakini single hii haikuwa na video yake.

Remove ads

Waimbaji

Onesho la moja kwa moja

Onesho la moja kwa moja, lilikuwa katika tamasha la Stand Up 2 Cancer lililofanyika tarehe 5 Septemba 2008, lililooneshwa katika vyombo vya habari mbalimbali. Waimbaji wengi walionekana ambao walirekodi wimbo huu isipokuwa, LeAnn Rimes, Sheryl Crow na Melissa Etheridge, na wapo walioongezeka kama vile Nicole Scherzinger kutoka katika kundi la Pussycat Dolls aliyeimba nafasi ya Sheryl Crow.

Orodha ya nyimbo

  1. "Just Stand Up!"
  2. "Just Stand Up!" (Live Video)

Chati

Wimbo huu uliingia katika chati ya Billboard Hot 100 katika wiki ya 78, ya tarehe 13 septemba. Wiki iliyofuatia ilifanikiwa katika mauzo na kuvuka nafasi takribani 67 na kufika hadi nafasi 11. Wiki iliyofuatia wimbo huu ulianguka na kushuka hadi nafasi na 36. Wimbo huu pia ulishaingia katika chati ya Uingereza na kufanikiwa kushika nafasi 39, na baadae kupanda hadi nafasi 26. Katika chati ya nchini Canada wimbo huu ulifanikiwa kufika hadi nafasi ya 10 katika wiki ya septemba 11.

Chati

Maelezo zaidi Chati (2008), Ilipata nafasi ...
Remove ads

Wafanyakazi

Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads