Kabari
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kabari (kwa Kiingereza wedge) ni chombo kinachotumiwa kwa kupasua kitu au gimba, pia kwa kutenganisha vitu viwili vilivyoshikamana. Umbo lake linafanana na pembetatu nyembamba.

Kifizikia inatumia kanuni za bapa betuko, hivyo inaitwa pia "mashine sahili".[1]
Matumizi ya kila siku ni kupasua shina la mti kuwa kuni au kupasua jiwe. Kimsingi hata uwezo wa kisu au shoka wa kukatia unafuata mfano wa kabari maana vyote hutegemea kanuni za bapa betuko.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads