Kadi ya picha

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kadi ya picha
Remove ads

Kadi ya picha (kwa Kiingereza graphics card) ni kifaa cha elektroniki kinachotumiwa na kompyuta ili kuchakata na kutoa picha kwenye monita. Kadi hii ina GPU (Kitengo cha Uchakataji Picha), kumbukumbu ya video, na sehemu za kuunganisha na bodimama kupitia PCI Express au AGP. Kadi za picha hutumiwa sana katika michezo ya video, uhariri wa video, muundo wa picha, na uchambuzi wa data.

Thumb
Kadi ya picha ya kisasa ya kiwango cha juu: Radeon RX 6900 XT kutoka AMD.
Remove ads

Muundo

Kadi ya picha ina vipengele kadhaa muhimu:

  • GPU (Kitengo cha Kuchakata Picha) – Hiki ndicho kiini cha kadi ya picha kinachochakata data ya picha.
  • Kumbukumbu ya video – Hifadhi ya muda inayotumiwa kuhifadhi data ya picha kabla ya kuonyeshwa.
  • Mfumo wa kupoza – Feni za na kupunguza joto zinazosaidia kupunguza joto la GPU.
  • Sehemu za kuunganishaHDMI, DisplayPort, VGA, na DVI kwa kuunganisha na monita.
Remove ads

Historia

Kadi za picha zilianza kama sehemu za msingi za kuonyesha maandishi kwenye skrini. Katika miaka ya 1980, IBM ilianzisha MDA na CGA, ambazo zilitoa picha za msingi. Miaka ya 1990 ilileta vichapuzi pembetatu kama Voodoo Graphics ya 3dfx, na baadaye NVIDIA na AMD zilianza kutawala soko la kadi za picha.

Matumizi

Kadi za picha hutumiwa katika:

  • Michezo ya video – GPU huwezesha uchezaji wa michezo yenye picha za hali ya juu.
  • Uhariri wa video – Programu kama Adobe Premiere Pro hutegemea GPU kwa uchakataji wa video.
  • Muundo wa pichaAutodesk Maya na Blender hutumia GPU kwa uundaji wa picha za 3D.
  • Uchambuzi wa data – GPU hutumiwa katika kujfiunza kwa mashine na AI kwa uchakataji wa data kubwa.[1]

Watengenezaji wakuu

Baadhi ya kampuni zinazotengeneza kadi za picha ni:

  • NVIDIA – Inajulikana kwa GeForce na RTX.
  • AMD – Inajulikana kwa Radeon.
  • Intel – Inatengeneza Intel Arc.

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads