Kaidi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kaidi (ing. na lat. Alkaid pia η Eta Ursae Maioris, kifupi Eta UMa, η UMa ) ni nyota angavu ya tatu katika kundinyota la Dubu Mkubwa (Ursa Maior).

Jina
Kaidi ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [1]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema hapa kwa kawaida القائد al-qaid ("kiongozi"); hii ni kifupi la jina ndefu zaidi قائد بنات النعش qaid banat al-na‘ash ("kiongozi wa mabinti wa jeneza", yaani kiongozi wa maombolezo au kilio). Klaudio Ptolemaio hakuwa na jina maalumu kwa nyota hii.[2]
Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulifuata mapokeo ya Warabu na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Alkaid" [3]. Eta Ursae Maioris (au η Ursae Maioris) ni jina la Bayer kufuatana na utaratibu ulioanzishwa na Mjerumani Johann Bayer katika karne ya 17. Bayer aliiona kuwa nyota angavu ya saba (hivyo inatajwa kwa herufi ya saba kwenye alafabeti ya Kigiriki) katika kundinyota la "Ursa Maior" (kwa Kiswahili Dubu Mkubwa) lakini hali halisi ni nyota angavu ya tatu katika kundinyota hili..
Remove ads
Tabia
Kaidi - Alkaid ina mwangaza unaoonekana wa Vmag +1.84. Mwangaza halisi ni −0.67. Hivyo iko kati ya nyota angavu zaidi 40 kwenye anga ya usiku.
Kaidi iko kwa umbali na Dunia wa miakanuru 100. Masi yake ni takriban M☉ 6 na nusukipenyo chake R☉ 3.4 (vizio vya kulinganisha na Jua letu) .
Ni nyota ya safu kuu katika kundi la spektra B3 V. Uso wake una joto kubwa mnamo nyuzi za Kelvini 16,823 na hivyo rangi yake ni nyeupe – buluu.
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya Nje
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads