Wilaya ya Kalambo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wilaya ya Kalambo ni wilaya mpya katika mkoa wa Rukwa yenye postikodi namba 55400, ambayo ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012.[1]
Makao makuu ya wilaya yako Matai.
Mkuu wa wilaya wa kwanza alikuwa Moshi Chang'a. [2]
Wilaya limepokea jina kutoka mto Kalambo unaopita hapa hadi kuishia kweye Maporomoko ya Kalambo upande wa Zambia.
Idadi ya wakazi wa wilaya ilikuwa 207,700 wakati wa sensa ya mwaka 2012. [3] Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 316,783 [4].
Remove ads
Uchumi
Eneo la Kalambo liko kati ya Sumbawanga mjini na mpaka wa Zambia. Barabara ni chache na mbaya. Wakazi wengi hulima na kufuga. Mazao ya sokoni ni pamoja na mahindi, alizeti, maharagwa, muhogo na asali.[2] Watu wachache wanalima madini na kuvua samaki.[2]
Utawala
Katika uchaguzi wa bunge la Tanzania Kalambo ni jimbo la uchaguzi.[5]
Kata
Wilaya ya Kalambo huwa na kata 17:[6]
|
|
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads