Mkoa wa Rukwa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mkoa wa Rukwa ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Uko kusini mashariki mwa nchi, ukipakana na Mkoa wa Katavi upande wa kaskazini, na mkoa wa Songwe upande wa mashariki, nchi ya Zambia upande wa kusini na huko magharibi Ziwa Tanganyika ndilo mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kabla ya kumegwa mwaka 2012 eneo la mkoa lilikuwa takriban km² 70,000. Kwa sasa lina kilomita ya mraba 27,765. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa wakazi 139,019 [1]. Kusini mwa mkoa liko ziwa Rukwa ambalo ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki na ndilo lililoupatia mkoa jina lake. Makao makuu ya mkoa ni Sumbawanga.

Remove ads
Wilaya
Wilaya ziko nne (katika mabano idadi ya wakazi mwaka 2022 [2].):
- Sumbawanga Mjini (303,986)
- Wilaya ya Sumbawanga (494,330)
- Wilaya ya Nkasi (425,420)
- Wilaya ya Kalambo (316,783).
Wilaya ya Mpanda ilikuwa sehemu ya Rukwa ikawa kiini cha mkoa mpya wa Katavi kuanzia mwaka 2012.
Wakazi
Kabila kubwa zaidi mkoani ndio Wafipa walioko hasa katika wilaya za Sumbawanga na Nkasi. Kati ya makabila mengine kuna Wamambwe-Lungu, Wawanda na Wanyamwanga katika wilaya ya Sumbawanga; kuna pia Wasukuma, Wanyamwezi na Wamasai. Kwa asilimia kubwa wakazi ni waumini wa Kanisa Katoliki.
Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads