Kamati
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kamati (kutoka neno la Kiingereza "committee") ni kundi la watu walioteuliwa au kuchaguliwa kwa ajili ya kazi maalum.
Makala hii inahitaji vyanzo zaidi ili kuwezesha kuonyesha uthibitisho. |

Mara nyingi huteuliwa miongoni mwa wajumbe wa kikundi au kundi kubwa na wakati mwingine hutarajiwa pia kufanya utafiti wa kina kuhusu jambo maalum kwa muda fulani na hatimaye kutoa mapendekezo kulingana na matokeo ya utafiti wao. Kwa mfano nchini Tanzania Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imeundwa chini ya Kanuni ya 118 (1) & (2) ikisomwa pamoja na fasili ya 1(c) ya Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016. Kwa mujibu wa fasili ya 4 (1) ya Nyongeza ya Nane, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imepewa majukumu yafuatayo: (a) Kuchunguza na kutoa mapendekezo kuhusu masuala yote ya haki, kinga na madaraka ya Bunge yatakayopelekwa na Spika; (b) Kushughulikia mambo yanayohusu maadili ya Wabunge yatakayopelekwa na Spika[1].
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads