Karani

From Wikipedia, the free encyclopedia

Karani
Remove ads

Karani (kutoka neno la Kiarabu قرا kusoma[1]) ni mtu ambaye hufanya kazi za ofisini katika taasisi za serikali au kampuni au mwajiri mwingine yeyote.

Thumb
Karani wa manispaa, mchoro wa Albert Anker, 1874.

Wajibu wa karani ni pamoja na utunzaji wa kumbukumbu na majukumu mengine ya kusaidia utawala. [2]


Historia

Neno clerk linatokana na neno la Kilatini clericus likimaanisha padri au mwana wa kanisa, ambalo ni tafsiri ya Kigiriki klērikos (κληρικός), lililotokana na neno linalomaanisha bahati au kura, na kwa maana hiyo pia mgawanyo au eneo la ardhi.[3][4]

Uhusiano huu ulitokana na mahakama za enzi za kati, ambapo kazi ya kuandika ilifanywa zaidi na makasisi kwa kuwa watu wengi wa kawaida hawakujua kusoma. Katika muktadha huo, clerk lilimaanisha msomi. Hadi leo, istilahi clerk regular bado inamtaja padri anayeishi kwa kufuata kanuni fulani za kidini. Katika baadhi ya lugha kama Kiholanzi, neno linalofanana, Klerk, mwishoni mwa karne ya 19 lilianza kutumika kumaanisha cheo cha chini katika mfumo wa kiutawala.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads